Msumbiji yapiga marufuku aina ya vipodozi hatari sana kwa afya

Aina mbalimbali za vipodozi vikiuzwa katika duka la vipodozi Seoul, Korea Kusini, Dec. 23, 2014.

Mamlaka nchini Msumbiji zimechona bidhaa 10,000 za vipodozi ambayo ni ‘hatari sana’ kwa afya kufuatia tahadhari kutoka Umoja wa Ulaya.

Bidhaa hizo ni pamoja na sabuni za maji za kuogea, shampoo krimu na zile za kupuliza.

Mamlaka inasema bidhaa hizo vitu ambavyo vinaweza kusababisha saratani, ikiongezea kuwa ni hatari kwa afya ya uzazi na pia vinaweza kusababisha kutokuwa na uwezo wa kushika mimba

EU ilionya dhidi ya matumizi ya bidhaa hizo mapema mwezi Septemba, alisema Sheila Mercis mkaguzi katika mamlaka ya kufuatialia dawa nchini humo ANARME.

FILE - Bunge la Umoja wa Ulaya

Watengenezaji wa bidhaa hizo tayari wamewasilisha aina mpya ya vipodozi ambavyo ANARME ilivitaja ili kupata idhini kusudi viwezei kuagizwa tena kutoka nje lakini vikiwa ‘havina vitu ambavyo ni hatari’ kwa binadamu.