Uhaba wa chakula kuhatarisha maisha Sudan

Watu waliopoteza makazi kutoka na vita vinavyoendelea Sudan wakisubiri kupokea misaada Desemba 23, 2023. Picha na AFP

Shirika la Chakula Duniani WHO limesema kwamba msimu ya uhaba wa chakula unaokaribia nchini Sudan heunda ukapelekea viwango vya juu vya njaa, magonjwa pamoja na vifo kutokana na magonjwa ya kuambukizwa miongoni mwa watu wenye njaa.

“Imekuwa miaka kumi tangu kuzuka kwa ghasia nchini Sudan, na kupelekea hali ya janga kubwa la kibinadamu,” amesema Peter Graaff Kaimu mwakilishi wa WHO, kwa ajili ya Sudan.

Akizungumza mjini Cairo Jumanne, Graaff aliwaamba wanahabari waliokuwa Geneva kwamba takriban watu milioni 25, ambao ni zaidi ya nusu ya wakazi wa Sudan wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Miongoni mwao, milioni 18 wanakabiliwa na njaa, wakiwemo milioni tano waliopo kwenye hali ya dharura, wakati wakiwa kwenye hatari ya kufa njaa. Huko Darfur, watoto laki mbili wanakadiriwa kukumbwa na njaa mwaka huu.

WHO limeonya kuwa hatua za haraka zinahitaji kuchukuliwa kwa kuwa msimu wa upungufu wa chakula umebaki wiki sita pekee. Huo ndiyo msimu ambapo hifadhi za chakula hushuka, kabla ya msimu mpya wa kuvuna kuingia.