Yunus alishinda tuzo huyo ya Nobel 2006 kutokana na ubunifu wake katika kutoa mikopo midogo kusaidia watu masikini, lakini akapewa kifungo cha miezi 6 jela, Januari mwaka huu kutokana na shitaka tofauti la kukiuka sheria za wafanya kazi, ambapo pia alipewa dhamana.
Mwongoza mashitaka Mir Ahmmad Ali Salam amesema kwamba kesi hiyo ya ubadhilifu inahusu mfuko wa hisani kwa wafanyakazi inaomilikiwa na kampuni ya mawasiliano ya Grameen Telecom ambayo inamiliki aslilimia 34.2 ya kampuni kubwa zaidi ya mawasiliano nchini humo.
Yunus pamoja na washitakiwa wengine 7 wamefikishwa mahakamni Jumapili, ingawa washukiwa wengine 6 hawakufika. Wakali wa washitakiwa Abdullah Al Mamun, aliambia mahakama kwamba Yunus mwenye umri wa miaka 83, pamoja na wenzake hawana hatia. Mwaka uliopita, zaidi ya viongozi 170 wa dunia, walisihi waziri mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina amuondolee Yunus kesi hiyo.