Mkutano mkuu unaangazia ushirikiano wa kibishara kati ya China na Afrika.
Mkutano wa mwaka huu unaangazia namna ya kukuza viwanda na usambasaji wa bidhaa kwa kuzingatia ruwaza ya ushirikiano kati ya China na Afrika ya mwaka 2035 na ajenda ya maendeleo ya Afrika ya m waka 2063.
Kongamano limevutia zaidi ya washiriki 1000, wakiwemo wawakilishi 400 wa taasisi na biashara mbalimbali kutoka nchi 48 za Afrika zikiwemo Kenya, Senegal, na Afrika Kusini.
Kongamano hilo limefunguliwa wakati kikao cha viongozi wa Afrika kinakamilika leo Ijumaa.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaambia viongozi wa Afrika kwamba ushirikiano mpana kati ya China na Afrika unaweza kupata suluhu ya nishati safi.
"Inaweza kuwa kichocheo cha mfumo muhimu wa chakula na digitali. Afrika ambao ni muhimu kwa uchumi wa nchi kadhaa duniani, inaweza kutumia fursa hiyo kupata msaada wa China katika kuimarisha biashara, usimamizi wa taarifa, fedha na teknolojia," alieleza zaidi Katibu Mkuu.