Mamia ya viongozi wa kisiasa na biashara wa Afrika walikusanyika katika ukumbi wa Great Hall of the People nchini China leo Alhamisi wakiwa na shauku ya kuunda ushirikiano mpya, kusaini mikataba na kuboresha uhusiano wa kiviwanda. Biashara ni biashara, tutanunua kutoka mahali popote.
Nchini China, bei ni nzuri,” Abakar Tahir Moussa, mmiliki wa kampuni ya ujenzi ya Chad aliliambia shirika la habari la AFP akionyesha kadi ya biashara ya mshirika mpya wa China.
Alitarajia kutumia Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, ambalo linamalizika kesho Ijumaa, kushirikiana na makampuni ya China katika miradi ya barabara na madaraja.
"Nipo hapa kufanya mawasiliano na kupata biashara zaidi", Moussa alisema baada ya kujiunga na maelfu ya wajumbe kutoka nchi zaidi ya 50 katika sherehe za ufunguzi wa jukwaa hilo.
Forum