Chaguzi Kenya zasababisha mkutano wa EAC kuahirishwa

Mwenyekiti wa EAC Rais John Magufuli

Mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliokuwa ufanyike Arusha, Tanzania umeahirishwa kwa mara ya tatu, na mara hii ikielezwa kuwa sababu ni mchakato wa chaguzi za awali zinazoendelea Kenya hivi sasa.

Marais kutoka nchi sita zinazounda EAC wameamua kuiachia Kenya, ambaye ni mwanachama muhimu, kumaliza mchakato wa uchaguzi unaoendelea wakati ikijitayarisha na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Agosti 2017.

Kwa hivyo mkutano ambao ulikuwa ufanyike hapa Jumatano, Mei 10, 2017 chini ya uwenyekiti wa Rais John Magufuli, hivi sasa utafanyika Jumamosi, Mei 20, 2017 ambao kuna uwezekano ukaahirishwa tena.

Repoti ya Sekretarieti ya EAC inasema kuwa, eneo la kwanza la Mkutano kwa sasa limebadilishwa kutoka Arusha, ambapo ilikuwa imependekezwa kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC) April 6, na sasa utafanyika Dar es Salaam wiki ijayo, kama tu tarehe hizo hazijabadilishwa.

Mwezi uliopita, Mkuu wa Mawasiliano na Mahusiano wa EAC, Mr Richard Owora Othieno alitangaza kuwa Mkutano wa EAC ambao ulikuwa ufanyike huko Arusha tarehe 6 April, 2017 ulifutwa kwa ajili ya kuiwezesha Burundi, ambayo huwa imetenga Aprili 6 kila mwaka kama ni “Siku ya Mauaji”.

Siku hiyo imetengwa na Burundi kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha Rais Cyprien Ntaryamira, ambaye pamoja na Rais Juvenal Habyarimana wa Rwanda waliuawa wakati ndege waliokuwa wakisafiri nayo kutoka Dar es Salaam ilipotunguliwa na watu wasiojulikana mwaka 1994.

Huko nyuma tarehe iliyokuwa imetengwa upya ya Mei 10 imebadilishwa hivi sasa kuwa Mei 20.