Mkutano wa COP29 wakosolewa, wataalamu wasema mazungumzo hayakidhi malengo 

Wanaharakati wakipinga ushawishi unaofanywa na mawakala wa wachimbaji mafuta na gesi wakati wa mkutano wa COP29 huko Baku, Azerbaijan

Kundi la viongozi wa zamani na wataalamu wa hali ya hewa  wanasema mazungumzo ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa ya hali ya hewa hayafai tena kwa malengo  yaliyoko.

Wanasema yanahitaji kufanyiwa mageuzi kama yalivyonukuliwa kutoka katika barua ya wazi ya ukosoaji ikiwa ni katikati ya Mkutano ambao hadi sasa umekuwa na mivutano.

Takriban nchi 200 zinakutana Baku, Azerbaijan kwa azma kuu ya kukubaliana juu ya lengo jipya ni kiasi gani cha pesa kinahitajika kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kumudu mabadiliko.

Hadi sasa mazungumzo hayo yamepiga hatua ndogo.

Barua ya leo iliyotiwa saini na wataalamu 20, viongozi wa zamani na wanasayansi akiwemo mkuu wa zamani wa UNFCCC, Christine Figueres na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon, na rais wa zamani wa Irelanda Mary Robinson.

Viongozi hao wamesema utaratibu wa COP umefikia pakubwa lakini sasa unahitaji mabadilko makubwa.