Waasi hao ni wa kundi la SPLM –N linaloongozwa na Abdelazizi al-Hilu na wanakadiriwa kufika maelfu ya wapiganaji wenye silaha nzito nzito.
Hadi sasa haijafahamika ni upande gani al-Hilu ataelemea katika mapigano yaliyoanza katika mji mkuu wa Khartoum Aprili 15 kati ya jeshi la taifa na kikosi cha dharura cha RSF.
Lakini wakazi wanasema kukusanya pamoja wapiganaji wake kunazusha hofu ya kuzuka mapambano.
Wakazi hao wanasema Wapiganaji wa SPLM-N wamekusanyika katika kambi za kijeshi karibu na Kadugli, mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kusini , na kusababisha jeshi la taifa kuimarisha vita vyake.
Na wanaongeza kusema kwamba wapiganaji wa RSF wamefunga barabara kati Kadugli na El Obeid upande wa kaskazini na kuzuia usafiri wa bidhaa.