Mivutano ya kikabila yaongezeka DRC

Vijana wa DRC wakishiriki katika kampeni za uchaguzi, Bukavu, DRC.

Kamishna wa ngazi ya juu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk ameonya kuhusu kuongezeka kwa mivutano ya kikabila na kuzitaja ghasia za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinatokana na mzozo wa uchaguzi.

Uchelewesho wa hali ya juu na vurugu za urasimu umeharibu uchaguzi wa rais, wabunge wa taifa na majimbo pamoja na madiwani.

Mpaka sasa Tume ya Uchaguzi imetangaza matokeo ya uchaguzi wa rais--- yaliyompa ushindi mkubwa rais aliyeko madarakani Felix Tshisekedi, matokeo ambayo upinzani umeyakataa kuwa ni ya udanganyifu.

“Nina wasiwasi mkubwa wa kuzuka kwa matamshi ya chuki za kikabila na uchochezi wa ghasia huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo” (DRC) amesema kamishna huyo wa Umoja wa Mataifa.

Alisema wito wa ghasia uliyotolewa baada ya uchaguzi ulikuwa una mashaka hususani na maeneo ya Kivu Kaskazini na Kusini – ambayo yamekubwa na makundi ya watu wenye siraha na mauaji ya kikabila – ikiwemo mikoa ya Kasai na Katanga.

Tshisekedi anatokea Kasai na Moise Katumba mmoja wa wapinzani wake wakuu anatokea Katanga.

Mivutano inayohusiana na uchaguzi ni kawaida DRC, ambayo ina historia ya utawala wa kimabavu na mapinduzi ya serikali yenye ghasia.

Makabila tofauti yapatayo 250 yanaishi katika nchi hiyo kubwa.

VOA