Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, matokeo ya uchaguzi yaliyotolewa na tume huru ya uchaguzi ya CENI kufikia Ijumaa yanaonyesha kuwa Rais Felix Tshisekedi anaongoza mbele ya wapinzani wake 18 kwa zaidi ya asilimia 72 ya kura takriban milioni 15.9 zilizopigwa wakati wa uchaguzi huo.
Mfanyabiashara mashuhuri Moise Katumbi na Martin Fayulu wapo kwenye nafasi za pili na tatu mtawalia wakiwa na zaidi ya asilimia 18 na asilimia 5 ya kura zilizopigwa. Kulingana na CENI, matokeo yaliyowasilishwa ni kutoka kwenye vituo 52,173 kati ya jumla ya karibu vituo 76,000 vilivyoko kote nchini.
CENI imekuwa ikitangaza matokeo hayo kutoka kwenye kituo maalumu mjini Kinshasa kwa jina ‘Basolo’ yaani ukweli kwa lugha ya Kilingala, kila siku tangu Desemba 22.
Forum