Russia imeshambulia kwa kutumia makombora tofauti wakati wa majira ya asubuhi yaliyokuwa na harakati nyingi, wakipiga majengo ya waakaazi na miundombinu ya raia.
Mamlaka za jeshi zilitoa onyo la mashambulizi ya anga ambalo lilidumu kwa saa tatu.
Shambulizi limekuja saa kadhaa baada ya rais wa Russia Vladmir Putin kusema shambulizi la anga katika mji wa Russia – Belgorod, halitapita bila kuadhibiwa. Moscow imesema shambulizi la anga limeuwa raia 24 na kuilaumu Ukraine.
Meya wa Kyiv Vitali Klitschiko amesema mwanamke mzee alikuwa katika gari la kubeba wagonjwa baada ya kujeruhiwa. Awali alisema kwamba takriban watu 16 wamejeruhiwa katika mji mkuu.
Mabomba yameharibiwa katika wilaya ya Pecherskyi huko Kyiv , na umeme na maji vimekatwa katika wilaya mbalimbali za mji mkuu.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.