Mgonjwa aliyepandikizwa figo ya nguruwe afariki katika hospitali ya Jimbo la Boston

Madaktari wa upasuaji wakimpandikiza figo ya nguruwe mgonjwa katika hospitali kuu ya Massachusetts, Machi 16, 2024. Picha ya AP

Mgonjwa wa kwanza aliye hai kupandikizwa figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba amefariki miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji, hospitali ya Marekani iliyofanya kazi hiyo imesema.

“Hospitali ya Mass General ina maskitiko makubwa kutokana na kifo cha bwana Rick Slayaman. Hatujaona dalili kwamba ni matokeo ya kupandikizwa figo hivi karibuni, “ hospitali ya jimbo la Boston ilisema katika taarifa iliyotolewa Jumamosi jioni.

Kwa mara ya kwanza ulimwenguni, madaktari wa upasuaji katika hospitali kuu ya mji wa Massachussets mwezi Machi walifanikiwa kupandikiza figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba ndani ya mwili wa Slayaman, ambaye alikuwa na umri wa miake 62 wakati huo na alikuwa na ugonjwa hatari wa figo.