Wafuasi wake walianza kusherekea mitaani baada ya siku ya amani ya uchaguzi ambayo wengi wanatumaini utaleta mabadiliko.
Mamilioni ya watu walijitokeza kumchagua rais wa tano wa Senegal kufuatia miaka mitatu ya msukosuko wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa na ambao ulichochea maandamano mabaya dhidi ya serikali na kuhimiza uungwaji mkono kwa upinzani.
Wapiga kura walitakiwa kumchagua mmoja kati ya wagombea 19 kuchukua nafasi ya Rais Macky Sall, ambaye anaachia ngazi baada ya muhula wa pili uliokumbwa na machafuko kutokana na kumfungulia mashtaka kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko na hofu kwamba Sall alikuwa na lengo la kurefusha muhula wake baada ya kikomo cha mihula kilichowekwa ndani ya katiba.
Rais aliye madarakani hakuwa kwenye orodha ya wagombea kwa mara ya kwanza katika historia ya Senegal.
Muungano wa vyama vinavyotawala ulimteua waziri mkuu wa zamani Amadou Ba, mwenye umri wa miaka 62 kama mgombea wake.
Hesabu za kwanza za kura zilizotangazwa kwenye televisheni zinaonyesha Faye atapata wingi wa kura, na kuchochea sherehe kubwa mitaani miongoni mwa wafuasi wa upinzani katika mji mkuu wa Dakar.
Matokeo ya mwisho yanatarajiwa Jumanne. Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika ikiwa hakuna mgombea atakayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zinazohitajika ili kuepuka marudio ya uchaguzi.