Kushindwa katika uchaguzi wa Jumamosi kunamaanisha kumalizika kwa utawala wa mihula miwili wa chama cha NPP chini ya uongozi wa Rais Nana Akufo-Addo, uliokabiliwa na mzozo mbaya wa uchumi, mfumuko mkali wa bei na kushindwa kulipa madeni.
“Wananchi wa Ghana wamezungumza, wananchi wamepiga kura ya mabadiliko kwa wakati huu na tunayaheshimu kwa unyenyekevu,” Bawumia alisema katika mkutano na waandishi wa habari. Alisema amempigia simu mpinzani wake mgombea wa Chama cha National Democratic Congress (NDC) na rais wa zamani John Mahama, kumpongeza.
Mahama amethibitisha kwenye mtandao wa X kwamba alipokea simu ya pongezi kutoka kwa Bawumia kutokana na “ushindi wake mkubwa.”