Meloni atarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza Italia wa mrengo mkali wa kulia

Giorgia Meloni

Giorgia Meloni anatarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza wa Italia wa mrengo mkali wa kulia tangu vita vya pili vya dunia.

Ameahidi kuwa kiongozi wa watu wote. Chama chake chenye siasa kali za mrengo wa kulia ‘Brothers of Italy’ na washirika wake wanatarajiwa kuwa na wingi wa viti katika mabaraza mawili ya bunge, kwa mujibu wa makadirio ya matokeo ya uchaguzi mkuu wa jana Jumapili.

Meloni, mwenye umri wa miaka 45, amesema atajitahidi kuuanganisha nchi yake kama atatakiwa kuunda baraza jipya.

Matokeo ya uchaguzi wa Jumapili unaonyesha kwamba anaweza kuwa mshindi na hivyo kuteuliwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo.

Meloni anaonekana akipunguza ukali wa siasa za mrengo wa kulia kwenye matamshi yake katika kile kinacho onekana ni juhudi za kuwahakikishia wanachama wa Jumuiya ya Ulaya na washirika wa kimataifa.