Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 18:10

Watu 14 wamefariki kwa ajali huko Italy


Polisi na timu ya uokozi wakiwa katika eneo la tukio huko Italy
Polisi na timu ya uokozi wakiwa katika eneo la tukio huko Italy

Mamlaka ilisema kwamba raia wa kigeni walikuwa miongoni mwa waliokufa, lakini hawajatoa maelezo zaidi. Picha kutoka eneo la tukio zinaonesha gari hilo likiwa limejifunga kwenye mteremko unaoelekea kwenye ziwa

Watu angalau 14 waliuawa Jumapili huko Italy, wakati gari moja maarufu la kubeba watalii lilipoanguka mita 20 kwenda chini. Miongoni mwa watalii hao alikuwa mtoto ambaye alifariki akiwa hospitali baada ya kupata mara mbili shinikizo la moyo.

Mtoto wa pili alijeruhiwa vibaya, lakini alikuwa na fahamu na uwezo wa kuongea, kulingana na taarifa za hospitali. Mamlaka ilisema kwamba raia wa kigeni walikuwa miongoni mwa waliokufa, lakini hawajatoa maelezo zaidi. Gari linalotumia waya la Stresa-Mottarone linasafiri kati ya mji wa Ziwa Maggiore hadi juu ya mlima Mottarone wa mkoa wa Piedmont nchini Italy kwa takribani dakika 20.

Picha kutoka eneo la tukio zinaonesha gari hilo likiwa limejifunga kwenye mteremko unaoelekea kwenye ziwa. Meya wa Stresa, Marcella Severino, aliliita eneo hilo ni la kutisha na alisema ajali hiyo inaweza kuwa imesababishwa na waya uliokatika.

XS
SM
MD
LG