Meli ya nafaka ya Ukraine yashambuliwa na kombora la Russia

Picha hii inaonyesha meli yenye bendera ya Panama iliyokuwa inaelekea kupakia nafaka katika Bahari ya Ukraine ya Black Sea

Meli yenye bendera ya Palau ilishambuliwa Jumatatu na kombora la Russia katika bandari ya kusini mwa Ukraine ya Odesa, kombora hilo liliua raia mmoja wa Ukraine na kujeruhi wahudumu watano katika shambulizi la pili kama hilo katika kipindi cha siku kadhaa, maafisa walisema.

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Andrii Sybiha alisema kwenye mtandao wa X kwamba meli mbili ziliharibiwa katika bahari ya Black Sea inayotumiwa kwa kusafirisha nafaka, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu hali ya shehena.

Alilaani vitendo vya Russia.

Wizara ya ulinzi ya Russia haijukibu mara moja barua pepe ya shirika la habari la Reuters ili kupata maelezo.

Moscow ilikanusha mara kadhaa kwamba inashambulia raia.

Gavana wa mkoa wa Odesa Oleh Kiper, akiandika kwenye mtandao wa Telegram, alisema mtu aliyeuawa katika shambulizi hilo alikuwa mfanyakazi wa bandari. Watano waliojeruhiwa ni raia wa kigeni na wahuhudumu katika meli hiyo.