Mazungumzo hayo mapya ni kati ya serikali ya Sudan Kusini na makundi ya upinzani ambayo hayakuwa sehemu ya makubaliano ya 2018 yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 5, ambapo zaidi ya watu 40,000 walikufa. Wakati mazungumzo hayo yakiitwa Tumaini, yalianza Mei, na pande zote zilikubaliana kudumisha amani. Hata hivyo yalikwama baada ya muda mfupi kufuatia rais Salva Kiir kufuta ujumbe wa serikali uliokuwa ukishiriki kwenye mazungumzo hayo.
Timu mpya iliteuliwa ili kuwakilisha upande wa serikali lakini haikuweza kufika Nairobi, kwa mara mbili mfululizo. Hakuna sababu iliyotelewa yao kutofika Nairobi, wala kilichopelekea kufukuzwa kwa ujumbe wa serikali wa awali. Wakati mkataba wa amani wa 2018 ukiwa bado haujatekelezwa kikamilifu, Sudan Kusini imeahirisha uchaguzi uliopangwa kufanyika Disemba mwaka huu hadi 2026.
Huo utakuwa uchaguzi kwa kwanza wa Sudan Kusini tangu kujipatia uhuru wake 2011. Sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa uchaguzi huo ilikuwa ni uandikishwaji wa wapiga kura pamoja na changamoto za kiuchumi, huku wafanyakazi wa serikali wakiwa wamehudumu kwa zaidi ya mwaka mmoja bila mishahara.