Hakuna aliyedai mara moja kuhusika na shambulio hilo, lakini tuhuma haraka ziliikumba Israel, ambayo ilikuwa iliapa kumuua Haniyeh na viongozi wengine wa Hamas kufuatia shambulio la kundi hilo la Oktoba 7, mwaka jana, dhidi ya Israeli, ambalo lilizua vita.
Mauaji ya Haniyeh mjini Tehran na shambulizi dhidi ya kamanda mkuu wa kundi la Hezbollah, Fouad Shukur, huko Beirut, yanaweza kuathiri juhudi za kupunguza mzozo wa Mashariki ya Kati, huku Iran pia ikitishia kujibu baada ya shambulio lililofanyika katika eneo lake.
Jeshi la Israel lilisema Alhamisi kwamba lilithibitisha kwamba mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas, Mohammed Deif, aliuawa katika shambulio la anga huko Gaza mwezi Julai.