Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:01

Maelfu wahudhuria mazishi ya kiongozi wa Hamas

Mazishi ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh na mlinzi wake ambapo Israel inalaumiwa kuhusika na mauaji wao. Mazishi yamefanyika leo Jumatano , Aug. 1, 2024, Tehran, Iran.
Mazishi ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh na mlinzi wake ambapo Israel inalaumiwa kuhusika na mauaji wao. Mazishi yamefanyika leo Jumatano , Aug. 1, 2024, Tehran, Iran.

Msafara wa mazishi ulifanyika kwa ajili ya kiongozi wa juu wa Hamas, Ismail Hanniyeh mjini Tehran leo Alhamisi.

Kiongozi mkuu wa Iran, na wawakilishi wa wanamgambo wa Palestina walilisalia jeneza la Ismail Haniyeh na mlinzi wake ambaye aliuawa katika mauaji ambayo Israel inalaumiwa kuhusika na kuna hatari ya kusambaa kwa vita katika kanda nzima.

Kiongozi wa Juu wa Kidini Iran Ayatollah Ali Khamenei akisalia jeneza la mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh, Tehran, Iran, Agosti 1, 2024.
Kiongozi wa Juu wa Kidini Iran Ayatollah Ali Khamenei akisalia jeneza la mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh, Tehran, Iran, Agosti 1, 2024.

Kituo cha televisheni cha serikali ya Iran baadaye kilionyesha majeneza yakiwekwa kwenye gari na kupitishwa mtaani kuelekea kwenye eneo la Azadi Square mjini Tehran na watu wakirusha maua kwenye majeneza hayo.

Baada ya ibada ya mazishi mjini Tehran, mwili wa Haniyeh unatarajiwa kupelekwa kwa maziko siku ya Ijumaa.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG