Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:58

Guterres anaonya mauaji ya kiongozi wa Hamas yanaweza kuzidisha taharuki Mashariki ya Kati


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumatano alionya kwamba Israel kumuua kamanda wa Hezbollah mjini Beirut na mauaji ya kiongozi wa Hamas mjini Tehran yanaashiria “uzidishaji hatari” wa hali ya taharuki huko Mashariki ya Kati.

Guterres alisema katika taarifa kwamba kipindi hiki “ juhudi zote zapaswa kujikita kwenye mchakato wa kufikia sitisho la mapigano katika vita vya karibu miezi 10 kati ya Israel na Hamas huko Gaza na kuongeza msaada wa kibinadamu kwa Wapalestina wanaokabiliwa na njaa, badala ya “kile tunachoona kama juhudi za kukwamisha malengo hayo.”

Guterres ametoa wito kwa pande zote “ kujizuia na uchochezi” lakini amekiri “kwamba kujizuia na uchochezi pekee yake haitoshi wakati huu mgumu sana.”

“Jumuia ya Kimataifa lazima ifanye kazi pamoja kuzuia haraka vitendo vyote ambavyo vinaweza kulitumbukiza eneo lote la Mashariki ya Kati katika mzozo, ambao utakuwa na athari mbaya kwa raia,” Guterres alisema.

Israel Jumanne jioni ilimuua kamanda wa Hezbollah, Fouad Shukr, katika shambulizi la anga kwenye moja ya majengo ya kundi hilo la wanamgambo katika mtaa wenye watu wengi mjini Beirut.

Israel ilisema Shukr alihusika na shambulizi la mwishoni mwa juma lililoua watoto 12 na vijana waliokuwa wanacheza mpira kwenye uwanja katika milima ya Golan iliyo chini ya udhibiti wa Israel.

Saa chache baadaye, Hamas ilisema kwamba Israel ilimuua kiongozi wake Ismail Haniyeh mjini Tehran, ambako Haniyeh alikuwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais mpya wa Iran.

Forum

XS
SM
MD
LG