Bi Mandela, ambaye alikuwa mmoja wa mashujaa waliopambana kidete na ubaguzi wa rangi na ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mke wa zamani wa rais wa kwanza wa nchi hiyo, Nelson Mandela, aliaga dunia tarehe mbili mwezi huu.
Mapema Jumamosi, maelfu ya wambolezaji walikusanyika katika uwanja wa Orlando, ulio mjini Soweto, kutoa heshima zao za mwisho katika hafla ambayo ilitajwa na shirika la habari la Reuters kama iliyoiunganisha mirengo yote ya kisiasa nchini humo.
Shirika hilo liliripoti kwamba marais wawili wa zamani wan chi hiyo, Thambo Mbeki na Jacob Zuma, pia wamehudhuria mazishi hayo.
Bintiye Winnie, Zenani Mandela-Dlamini, ni kati ya waliotoa hotuba wakati wa maziko hayo. Viongozi waliohudhuria maziko hayo ni pamoja na marais wa Jamhuri ya Congo, Namibia, na wanaharakati wa haki za raia kutoka ulimwenguni kote, akiwemo Mchungaji Jesse Jackson kutoka Marekani.
Aidha mazishi hayo yamehuduriwa na waombolezaji kutoka maeneo nchi mbalimbali ulimwenguni kote. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, alikuwa wa kwanza kutupa mchanga kwenye kaburi la Winnie Mandela.
Jeneza la Winnie lilifunikwa na bendera ya Afrika Kusini, huku baadhi ya waombolezaji wakivalia nguo zenye rangi ya chama cha African National Congress (ANC).
Mazishi hayo yalihitimisha siku 10 za maombolezo ya kitaifa, kipindi ambacho kiliwapa fursa maelfu ya watu kuutoa heshima zao za mwisho nyumani kwa Winnie, ambaye alifahamika na wengi kama Mama wa taifa.
Mpiganiaji huyo wa ukombozi alifariki akiwa na umri wa miaka 81. Mapema Jumamosi, waombolezaji walifuata jeneza lake katika maandamano yaliyoelekea kwenye uwanja wa mpira, ambapo maombolezo hayo yalianza kwa nyimbo ya taifa.