Matayarisho ya maziko ya Rais mstaafu George H.W. Bush
Rais mstaafu wa Marekani George H. W. Bush alifariki siku ya Ijumaa iliyopita huko Texas, Marekani
Kikosi maalum cha kumlinda Rais wa Marekani wakiwa wamebeba jeneza la Rais mstaafu George H.W Bush katika nyumba ya kutayarisha maiti baada ya familia kufanya maombi, Jumatatu, Desemba 3, 2018, huko Houston. Jumatatu, Desemba 3, 2018, huko mjini Houston. (AP Photo/Kiichiro Sato)
Rais Donald Trump akizungumza na vyombo vya habari juu ya kifo cha Rais mstaafu George H. W. Bush, wakati alipokutana na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel katika mkutano wa G20, Jumamosi, Desemba 1, 2018, huko Buenos Aires, Argentina. (AP Photo/Pablo Martinez Monsivais)
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel akizungumza na vyombo vya habari juu ya kifo cha Rais mstaafu George H.W. Bush wakati alipokutana na Rais Donald Trump, katika mkutano wa G20, Jumamosi, Desemba 1, 2018, huko Buenos Aires, Argentina.(AP Photo/Pablo Martinez Monsivais)
Bendera ya Marekani ikiwa inapepea nusu mlingoti mbele ya Bunge la Marekani ikiwa ni sehemu ya maombelezi ya kifo cha Rais mstaafu wa Marekani George H. W. Bush, mapema Desemba 2, 2018, mjini Washington.
Rais George H. W. Bush (kushoto) akiwa na Rais wa iliyokuwa Soviet Union Mikhail Gorbachev baada ya kumaliza mkutano wao na waandishi wa habari Moscow Julai 31, 1991
Sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kumbukumbu ya Rais George H.W. Bush ikiwa katika eneo la njia ya wanaotembea kwa miguu, Makazi ya familia ya Bush kipindi cha joto, Jumamosi, Desemba 1, 2018, mjini Kennebunkport, Jimbo Maine.
Kadi yenye ujumbe wa maombolezi ya kifo cha Rais George H. W. Bush
Mauwa na kadi zenye kuelezea kuwa Rais George H.W. Bush, aliyefariki Ijumaa kuwa ni mtu mwema.