Mauaji ya halaiki yaongezeka Myanmar

Polisi wakifanya doria Julai 19 2023, Siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya viongozi wa uhuru akiwemo jenerali Aung San, baba yake Aung San Suu Kyi. Picha na AFP

Jeshi la Myanmar liliongeza matumizi yake kwa mauaji ya watu wengi, mashambulizi ya anga na mizinga katika kipindi cha mwaka uliopita wakati likipambana kuzima upinzani dhidi ya wanaopinga mapinduzi yake, ofisi ya haki ya Umoja wa Mataifa ilisema Jumanne.

Jeshi kuiondoa serikali ya Aung San Suu Kyi mwaka 2021 kulizua mzozo mkubwa, na sasa jeshi linapambana na wapinzani katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu (OHCHR) imegundua "msururu wa ghasia za kijeshi" kati ya mwezi Aprili 2022 na Julai 2023, ilisema katika ripoti yake ya hivi karibuni kuhusu Myanmar.

Kupitia mahojiano na chanzo huria cha data, iligundulika "kuongezeka kwa kasi" ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu "ikiwa ni pamoja na ongezeko ... la matukio ambapo watu kumi au zaidi waliuawa".

Mpaka sasa wachunguzi wameorodhesha matukio 22 ya mauaji ya watu kumi au zaidi, kulingana na mkuu wa haki za binadamu, Volker Turk.

OHCHR ilitoa mfano wa shambulio la anga kwenye mkutano uliofanyika katika kijiji kwenye ngome ya upinzani mwezi Aprili, na kusema kuwa watu wapatao 150 waliuawa, na shambulio la bomu la Oktoba mwaka jana katika tamasha la waasi lililofanyika kaskazini mwa jimbo la Kachin ambako dazeni ya watu waliuawa.

Mara kwa mara, wanajeshi wamekuwa wakifanya vitendo vya ubakaji na mauaji holela kwa wanaume, wanawake na watoto katika vijiji vinavyoshukiwa kuwahifadhi au kuwaunga mkono wapiganaji wanaopinga mapinduzi, kulingana na OHCHR.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP