Mashambulizi ya makombora ya Russia ya usiku kucha dhidi ya miundombinu ya nishati yamesababisha kukatika kwa umeme katika mikoa ya Ukraine ya Sumy na Kharkiv inayopakana na Russia, wizara ya nishati ya Ukraine imesema Jumatatu.
Moscow ilizidisha mashambulizi dhidi ya vituo vya nishati katika miezi ya hivi karibuni, na kusababisha kukatika kwa umeme na mgao wa umeme nchini kote.
“Wakati wa usiku, adui alishambulia miundombinu ya nishati katika mkoa wa Sumy. Zaidi ya kaya 400,000 huko Sumy na miji mingine na vijiji vya mkoa huo havina huduma ya umeme,” wizara hiyo imesema.
Usambazaji wa umeme umerejeshwa katika baadhi ya maeneo” asubuhi,” wizara hiyo imeongeza.