Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Ijumaa imelaani tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
“Marekani imesikitishwa sana kuhusu kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, Mbunge na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika. Tunalaani kitendo hiki cha kipuuzi na cha kutumia nguvu. Tunaungana na Watanzania kutoa matumaini yetu ya dhati ili apone haraka," taarifa ya Ubalozi imesema.
Ubalozi huo umesema unaungana na Watanzania katika kumtakia kheri Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ili apone haraka.
Lissu jana Alhamisi saa sita usiku alisafirishwa kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya.