Marekani yahitajia msaada wa washirika wake kupambana na ujasusi wa China

Ujumbe wa Marekani, akiwemo Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Robert Lighthizer (wapili kulia) na Waziri wa Biashara Wilbur Ross (kulia) wakiwa katika mazungumzo na ujumbe wa China wakiwa na naibu Waziri Mkuu Liu He (wapili kushoto) Washington, DC, Januari 30, 2019

Maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani na wataalam wanasema kuwa Marekani inalazimika kuwahamasisha washirika wake wote kuishinikiza China iache kuiba teknolojia ya kiwango cha juu kupitia ujasusi wa mitandao.

Wakati huohuo, wabunge maarufu wa Marekani wanadadisi utayari na uwezo wa Marekani kukabiliana na ujasusi wa aina hiyo.

Msukumo huo mpya umetolewa baada ya waendesha mashtaka wa serikali kuu ya Marekani kushinikiza kufunguliwa mashtaka dhidi ya kampuni kubwa kuliko zote duniani ya mawasiliano – China Huawei Technologies – Mkuu wa Idara ya mahesabu na makampuni kadhaa tanzu kwa madai ya wizi wa fedha na wizi wa haki miliki za kazi za uvumbuzi.

“Tukio hilo linalo ihusisha kampuni ya Huawei inaonekana kama vile ni hatua dhidi ya kampuni moja, lakini suala ni kubwa kuliko hilo,” amesema Hu Xingdou, mwanazuoni aliyeko Beijing.

“Hii ni vita kati ya teknolojia ya nchi moja dhidi ya nchi nyingine, ni suala la nchi gani itakuja kushikilia nafasi ya juu katika ulimwengu wa teknolojia siku za usoni.”

Uongozi wa Trump, hata hivyo, unasema Washington inakerwa sana juu ya uwezekano wa Beijing kutumia makampuni ya teknolojia ya China kufanya ujasusi dhidi ya Marekani na washirika wake.

Wakati huo huo, Marekani na China wameanza mazungumzo ya kibiashara Jumatano huku wachambuzi wakisema kuna matumaini madogo ya kufikiwa ufumbuzi kwa kile kinachoelezewa na wachambuzi kuwa hilo ni kutokana na masharti ya Washington katika kushinikiza mageuzi katika mfumo wa kiuchumi wa China.

Mkutnano huo unafanyika Washington kwa yakiwa ni mazungumzo ya ngazi ya juu kabisa kuitishwa tangu Rais Donald Trump na Rais wa China Xi Jinping kukutana mwaka 2018. Mvutano wa kibiashara huo kati ya mataifa hayo umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa sasa.