Marekani yaahidi msaada wa dola milioni 133 kwa Haiti

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akishiriki mkutano wa nchi za Caribbean nchini Jamaica, Machi 11, 2024. Picha ya Reuters

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Israel Katz Jumatatu aliliomba Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa “kuongeza shinikizo kwa Hamas kadri iwezekanavyo” kuwaachia huru watu ilioshika mateka katika shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel.

Akihutubia mkutano wa dharura wa nchi za eneo la Caribbean huko Jamaica, Blinken alisema Marekani itatoa msaada mwingine wa dola milioni 100 kwa kikosi cha kimataifa na msaada mwingine wa kibinadamu wa mara moja wa dola milioni 33, na hivo ahadi za jumla za Marekani kwa Haiti zikiwa sawa na dola milioni 333.

Haiti imekumbwa kwa miongo kadhaa na umaskini uliokithiri, majanga na mzozo wa kisiasa lakini mambo yamekuwa mabaya zaidi tangu kuuawa kwa rais Jovenel Moise mwaka wa 2021.

Magenge ya wahalifu wenye silaha yanayodhibiti sehemu kubwa ya nchi na sehemu kubwa ya mji mkuu yalizidisha mashambulizi tangu wiki iliyopita.