Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Mike Pompeo amesema Ijumaa Washington imeanza utaratibu wa kufungua ubalozi mdogo katika Sahara ya magharibi.
Hatua hii imechukuliwa na serikali ya Marekani ikiwa ni wiki chache tu baada ya utawala wa Trump kutambua rasmi madai ya Morocco ya kumiliki koloni hilo la zamani la hispania.
Koloni hilo linalogombaniwa na chama cha ukombozi cha Sahrawi.
Taarifa ya Pompeo inaeleza kwamba ubalozi huo mdogo ambao hautakuwa na mtu huko utasimamiwa na ubalozi wa Marekani nchini Morocco.