Mapambano yazuka tena Jerusalem karibu na msikiti wa al-Aqsa

Msikiti mtakatifu wa al-Aqsa

Mwanadamanaji wa Kipalestina akiruka vizuizi vinavyo waka moto wakati wa maandamano dhidi ya Israeli kutokana na mvutano uliopo Jerusalem, karibu na makazi ya Wayahudi ya Beit El karibu na Ramallah, katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel, Ukingo wa Magharibi, Mei 9, 2021.

Vikosi vya usalama vikikabiliana na Wapalestina waliokuwa katika msikitini wakifanya ibada.

Vikosi vya usalama vya Israeli vikilinda doria wakati mvutano kati ya Waisraeli na Wapalestina ukiendelea katika maadhimisho ya Mayahudi ya Siku ya Jerusalem, karibu na eneo la Damascus Gate nje kidogo ya eneo la Old City, Jerusalem Mei 10, 2021. REUTERS/Ronen Zvulun

Mwanamke wa Kipalestina akiwa karibu na vikosi vya usalama vya Israeli wakati wa machafuko kati ya Waisraeli na Wapalestina huku Israeli ikiadhimisha Siku ya Jerusalem, katika eneo la Damascus Gate nje ya mji wa Old City, Jerusalem,  Mei 10, 2021. REUTERS/Ronen Zvulun

Wapalestina wakijihami baada ya vikosi vya usalama vya Israeli kutupa maguruneti, Mei 9, 2021. (Foto: Ronen Zvulun/Reuters)

Wapalestina wakikabiliana na vikosi vya usalama vya Israel katika ghasia zinazo endelea Jerusalem.

Mapambano mapya yamezuka Jumatatu kati ya vikosi vya usalama vya Israeli na Wapalestina waliokuwa wanafanya ibada karibu na msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem Jumatatu.