Katika kambi moja yenye msongamano mkubwa, kwenye mji mkuu wa Mogadishu watu waliofika hivi karibuni walikuwa na uchungu waziwazi walipoelezea walivyoshuhudia wana familia wakifariki na kuwaacha wapendwa wao nyuma walio hatarini.
Ukame hivi sasa unatishia mji mkuu wa somalia wakati kambi katika mji huo zikikabiliwa na wingi wa watu wanaowasili.
Kwa mujibu wa data zilizotolewa kwa shirika la habari la AP takriban watu 30 wamekufa hadi mwezi April.
Taarifa zinasema takriban watu 448 wamekufa nje ya vituo vya tiba vya utapiamlo na ndani ya vituo hivyo, kote nchini somalia mwaka huu hadi mwezi April.
Idadi hiyo inazingatia data ambazo hazikuripotiwa zilizotolewa na makundi ya kibinadamu na maafisa wa ndani na kutolewa katika shirika la AP.
Zaidi ya watu laki mbili nchini somalia wanakabiliwa na njaa kali ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka makadirio ya mwezi April .