Tangu Saied kunyakuwa mamlaka yote mwaka 2021, wakosoaji kadhaa, wakiwemo wanawake walikamatwa.
“Kwa bahati mbaya, leo ni siku ya hasira kwa wanawake waliofungwa jela kwa sababu ya maoni yao ya kisiasa na uanaharakati wao katika jamii,” alisema Karima Brini, kiongozi wa The Women and Citizen Association.
“Tuna hasira na tunaomba uhuru kwa wanawake wanaoshikiliwa,” aliongeza.
Wafuasi wa chama cha Free Destouriian walikusanyika pia karibu na wizara ya wanawake mapema Jumanne, wakiomba kuachiliwa kwa kiongozi wa chama, Abir Moussi, ambaye amefungwa jela tangu mwezi Oktoba.
Akiwa mkosoaji mkubwa wa Saied, Moussi alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani wiki iliyopita, siku mbili baada ya kuwasilisha fomu yake ya kugombea urais kwenye uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.