Wilaya ya Nsanje iliyoko kusini mwa Malawi kwa sasa inaongoza kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wa COVID 19 wanaojulikana mwaka huu.
Msemaji wa ofisi ya afya ya wilaya George Mbotwa, amesema wilaya imewaandikisha wagonjwa 17 katika kipindi cha wiki tatu zilizopita na baadhi yao ni wahudumu wa afya.
Ilipofika siku ya Jumatatu, Malawi imeorodhesha wagonjwa 89,202, ikiwa ni pamoja na vifo 2,686, tangu mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi April 2020.
Waziri wa Afya wa Malawi amesema kampeni mpya ya chanjo itasaidia kuongeza idadi ya watu waliopata chanjo ya COVID-19. Kiwango cha watu waliochanjwa katika baadhi ya maeneo ya Malawi kiko chini ya asilimia 40.