Kesi hizo zilizowasilishwa mbalimbali mjini New York, California, DC na majimbo mengine 11, zimeongeza mapambano ya kisheria dhidi ya TikTok inayomilikiwa na China na wadhibiti wa Marekani, na kutafuta adhabu mpya za kifedha dhidi ya kampuni hiyo.
Majimbo hayo yanaishtumu TikTok kutumia kwa makusudi programu ambayo imegeuka kilevi iliyoundwa ili kufanya watoto kutizama maudhui ya mtandao huo kwa muda mrefu na mara nyingi iwezekanavyo na kupotosha ufanisi wake katika kudhibiti maudhui.
TikTok inataka kuongeza muda ambao watumiaji wanatumia kwenye program hiyo ili kuwalenga na matangazo, majimbo hayo yamesema.
TikTok ilisema Jumanne kwamba haikubaliani kamwe na madai hayo,” mengi kati yake tunaamini kuwa sio sahihi na yanapotosha,” na kwamba imesikitishwa na kuona majimbo hayo yameamua kushtaki “badala ya kushirikiana nasi kwa kutafuta suluhisho mbadala kwa changamoto za tasnia nzima.