Mahitaji ya dawa za asili Eswatini yahatarisha kutoweka kwa wanyama pori

Wanyama wenye magamba ni mojawapo ya wanyama wanaotumiwa kwa dawa za asili

Dawa za asili au ‘muti’ ni sehemu muhimu katika utamaduni wa Eswatini. Hata hivyo, kuna ongezeko la mahitaji ya muti na kuliweka taifa hilo la kialme la kusini mwa Afrika kuwa katika hatari ya kupoteza wanyama wake.

Mwanabaiolojia Zamekile Bhembe, ambaye anafanya katika shirika la maabara ya EWild katika chuo kikuu cha Eswatini ambayo inafadhili na USAID, anapambana na majangili wanaojaribu kuwakamata na kuwashtaki kwa uhalifu wao.

Anasema ujangili kwa ajili ya malengo ya kutengeneza dawa za kienyeji ndiyo sababu kuu ya kushuka kwa viumbe hai na kutaka kanuni kanuni zipitishwa kuwalinda wanyama pori.

“Kila mara unapoona idadi ya viumbe hai ikishuka, kutakuwa kuna aina fulani ya ujangili. Kama nchi, hatuwezi kulikana hilo kuwa tunatumia rasilimali zatu kwa ajili ya dawa za kienyeji. Tunahitaji kubuni njia ya kupitisha kanuni za ufuatiliaji.” Bhembe.

kwa vizazi kadhaa, watu wa Eswatini wamekuwa naimani za kieneyeji na thamini ambazo ziko ndani ya mioyo yao. Hii ni kweli kwa zaidi ya asilimia 80 ya watu bado bado wanakwenda kupata ushauri kwa waganga wa kienyeji au na pia kutibiwa.

Waganga wa kienyeji wanatumia aina mbali mbali za mimea na wanyama kutengeneza dawa za kiasili, na wanatumia ujuzi waliopatiwa na vizazi vilivyopita. Hat ahivyo, uwindaji mkubwa umehatarisha jamii ya kakaona, mamba, ndege na bundi na hivyo kutolewa wito wa kuwa na mikakati endelevu kuzuia hali hii.

Makhanya Makhanya ni rais wa chama cha waganga wa kienyeji anayejulikana sana kwa kutoa tiba za kienyeji anasema jukumu la waganya wa kienyeji linahitaji kulindwa.

Amesema wamevihudumia vizazi kwa vizazi katika taifa hilo, kuwapatia dawa wale wenye shida. Hat ahivyo, sheria za sasa hazionyeshi ukweli wa kazi yao. Tunahitaji kanuni ambazo zitatambua kuwa jukumu letu kama jamii na kuturuhusu kuendelea kuwahudumia watu wetu.

Kwa njia yoyote ile, mustakbali wa dawa za asili huko Eswatini ni kuwa na uwiano mzuri. Kwa upande mmoja, kuna wale ambao wanatetea uhifadhi wake kama sehemu muhimu kwa urithi wan chi. Kwa upande mwingine, kuna wale ambao wanadai kwamba kuiweka katika hali ya sasa na kuwalinda wanyama pori ni vyema iwe ni kipaumbele.

Katikati ya haya ni mjadala wa idadi ya wanyama pori walio hatarini kupotea. Kwa kuweka uwiano kati ya utamaduni na maendeleo ambayo yanaweza kuhakikishiwa katika siku za usoni.