Hii inasubiri mahakama kusikiliza ombi la wakazi watatu wa Kisumu. Kupitia mawakili wao Kenneth Amondi, Titus Alila, Jackline Otieno na Francis Ogada, waliomwambia Jaji Stephen Riechi kuwa kodi mpya zitapandisha gharama za maisha.
Uamuzi wa mahakama hiyo tayari hivi sasa umeleta mkanganyiko. Jumanne Septemba 4, 2018, Mahakama Kuu ya Nairobi Chacha Mwita alikataa kusitisha kwa muda kodi hiyo kwa misingi ya kuwa mchakato wa utungaji wa sheria hiyo ulikuwa haujamalizika kwa sababu Rais Uhuru Kenyatta alikuwa hajatia saini msuwada huo au aliutupilia mbali Muswada huo mwaka 2018.
Wachambuzi wa mambo ya biashara nchini Kenya wanasema bei za mafuta katika vituo vya mafuta kuna uwezekano mkubwa zisibadilike kufuatia matangazo yaliyo tolewa na Tume ya Kusimamia Nishati (ERC) Septemba 1, 2018
“Japokuwa hili litabadilika iwapo marekebisho ya muswada wa fedha wa 2018 kama ulivyopitishwa na Bunge ukipitishwa kuwa sheria, mchakato wa bei za mafuta kwenye vituo itarekebishwa..” limesema tamko kutoka ERC Jumamosi.
Kufuatia kodi hiyo mpya, nchi imeshuhudia uhaba wa mafuta kwani wasambazaji wa mafuta wamekataa kuchukua mafuta kutoka kwenye depo za mafuta ikiilazimisha serikali kutoa ulinzi kwa wasambazaji hao wakuu.