Zuma aliondoka madarakani mwaka 2018, akiandamwa na tuhuma za ufisadi, alifungwa jela kwa muda kwa kuidharau mahakama. Tangu wakati huo alianzisha chama cha kushindana na chama cha African National Congress cha mrithi wake Cyril Ramaphosa.
Chama cha ANC kimeshinda kila uchaguzi wa Afrika Kusini tangu nchi hiyo kuwa ya kidemokrasia mwaka 1994, na Zuma alihudumu kama rais wa nne wa chama kati ya 2009 na 2018.
Lakini enzi yake iligubikwa na tuhuma za ufisadi zinazoandama vuguvugu la zamani la kupinga ubaguzi wa rangi, na mamlaka za uchaguzi zilidai kwamba hukumu ya Zuma ya 2021 inamzuia kugombea.
Zuma na chama chake kipya, uMkhonto Wesizwe, tawi la zamani la kijeshi la ANC, walipinga uamuzi huo ambao sasa umeidhinishwa na mahakama ya katiba.
Uamuzi wa Jumatatu unaweza kuwa na athari kubwa zenye misukusuko ya kisiasa.
Chama cha ANC cha Ramaphosa bado kina uhakika wa kuendelea kuwa chama kikuu nchini Afrika Kusini baada ya uchaguzi wa Mei 29, lakini baadhi ya kura za maoni zinaonyesha kuwa huenda kwa mara ya kwanza kikasumbuka kupata wingi wa kura.