Takriban watu 18, wakiwemo raia wa kigeni, walifariki na wengine wanne kutoweka baada ya mafuriko kusini mwa Morocco, wizara ya mambo ya ndani ilisema Jumatatu, ikisahihisha idadi ya awali ya watu 11 waliokufa.
10 kati yao walifariki katika mkoa wa Tata na watatu huko Errachidia, akiwemo raia wa Canada na mwingine wa Peru, wizara hiyo ilisema. Iliongeza kuwa watu wengine wawili walipoteza maisha huko Tiznit, wawili huko Tinghir, akiwemo raia wa Uhispania, na mwingine alifariki huko Taraoudant.
Wizara hiyo haikufafanua ikiwa raia hao wa kigeni walikuwa wakazi au wageni.
Tangu siku ya Ijumaa, maeneo yenye ukame kusini mwa Morocco yamezama katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa, maafisa walisema.