Watu 15 wamepoteza maisha baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi huko Kaskazini mwa Vietnam.
Kitengo kinachosimamia maafa Vietnam kimesema kuwa watu wasiopungua 11 hawajulikani waliko. Nyumba, mazao na barabara zimeharibiwa kabisa.
Kitengo hicho cha Maafa kinasema mvuo hizo zimesababisha hasara ya zaidi ya dola milioni 6.
Katika tamko lao, kitengo cha Maafa kimeripoti kuwa wahanga wa gharka hiyo kutoka katika majimbo yaliyokuwa milimani ikiwemo Lai Chau, Ha Giang na Dien Bien ambako mafuriko na maporomoko yametokea pia yamewajeruhi watu watano. Kitengo hicho kimeongeza kuwa idadi ya watu waliokufa inaweza kuongezeka.
Maafa hayo yanayotokana na hali ya hewa ambayo yameuwa mamia ya wananchi wa Vietnam kila mwaka, na kusababisha hasara ya mamilioni ya dola katika miundombinu na kilimo.