“Idadi ya vifo ni 30, msemaji wa idara ya kitaifa ya kusimamia majanga (NEMA) Ezekiel Manzo aliiambia AFP, siku moja baada ya maji kutoka kwenye bwawa lililojaa kusomba maelfu ya nyumba katika mji mkuu wa jimbo la Borno.
Mfanyakazi mwingine wa idara hiyo, Zubaida Umar alisema “Hali huko Maiduguri inatisha sana.”
Alisema mafuriko yaliteketeza asilimia 40 ya mji wote, na watu walilazimika kuondoka kwenye nyumba zao na wametawanyika kila mahali.
Umar alisema takwim walizonazo ni kwamba kuna watu 414,000 waliohama makazi yao.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi nchini Nigeria lilisema Jumanne kwenye mtandao wa X kwamba mafuriko hayo yalikuwa moja ya mafuriko mabaya kuukumba mji huo katika kipindi cha miaka 30.