Raia wa Cameroon watapiga kura mwaka ujao kumchagua rais kwa muhula mwingine wa miaka saba. Chaguzi za awali katika taifa hili la Afrika ya Kati zilikumbwa na taarifa potofu ambazo zilichochea machafuko kwenye mitandao ya kijamii.
Waandishi na Wataalamu Wachukua Hatua
Sasa, waandishi wa habari na wataalamu wa vyombo vya habari
wanasema wanachukua hatua za mapema ili kuzuia kurudiwa kwa masuala haya. Amboh Vanessalizzy, mtayarishaji wa Maudhui huko Buea, alikuwa akipitia mitandao ya kijamii wakati habari zilipoibuka kuwa rais wa Cameroon, Paul Biya, amefariki.
Bila njia yoyote ya uthibitisho, alisubiri mawasiliano rasmi hadi serikali ilipotoa
taarifa ya kukanusha uvumi wa kifo cha Rais kama ndoto tu,
Amboh Vanessalizzy, Mtengenezaji Maudhui asema:Kwa kadiri tunavyotaka mabadiliko, simuombei kifo mtu yeyote.
Taarifa Potofu Kama Zile Zinazomhusu Rais
Taarifa potofu kama zile zinazomhusu rais zinaweza kuwa za mara kwa mara, hasa wakati wananchi wa Cameroon wakielekea kwenye uchaguzi mwaka ujao.
Batata Boris-Kaloff]], Meneja wa Kituo cha CBS Buea aeleza:
"Tayari ninajitayarisha kukabiliana na taarifa potofu za uchaguzi ambazo
zinaweza kuja. Uwe na uhakika, huko Buea, kuna wanasiasa na kutakuwa na
mijadala kuhusu miradi hapa na pale."
Mhariri Mkuu wa DMRTV Buea
Jude Mbaku ni mwanahabari mwingine, na mhariri mkuu wa DMRTV Buea,
mkaguzi mkuu wa kuhakiki habari za kweli katika eneo ambalo hapo awali
liliathiriwa na habari potofu. Mbaku anasema ameona makundi yanayotumia
mitandao ya kijamii kupotosha umma, na matokeo yake ni makubwa.
Jude Mbaku wa DMRTV Buea -Mhariri Mkuu anasema: Timu ya Cameroon ilipokwenda Cote d’Ivoire kwenye michuano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika, tetesi zilienea kwamba Njie Clinton amejiuzulu kwenye
kikosi. Na walioeneza habari hizi walikuwa wapiganaji waliojitenga. Hili
halikufanywa kama jambo la makosa. Ilikuwa imeandaliwa vizuri na
kutayarishwa vyema ili kupotosha watu.
Waandishi Cameroon Wakabiliwa na Changamoto Nyingi
Karloff anasema kuwa waandishi wa habari wa Cameroon wanakabiliwa na
changamoto nyingi katika kuripoti kwa usahihi, ikiwa ni pamoja na ufadhili
mdogo, hatari za usalama, na upatikanaji mdogo wa habari.
Boris-Kaloff Meneja wa kituo cha CBS Buea anatoa maelezo zaidi:
"Nchini Cameroon, ni vigumu kupata takwimu na data. Unajua, nimekwenda
kwa wajumbe wa kanda wa usafiri kuulizia takwimu za magari yaliyosajiliwa
kusini-magharibi, haswa huko Buea, na nikaambiwa niende kusimama
barabarani kuanza kuhesabu magari mimi mwenyewe."
Profesa Kingsley Ngange wa Fulbright
Licha ya changamoto hizo, wataalamu kama vile Profesa Kingsley Ngange, msomi wa Fulbright na mkufunzi wa uandishi wa habari, wanasisitiza umuhimu wa kujuakusoma na kuandika kwa vyombo vya habari na kuripoti maadili.
Profesa Kingsley Ngange, Mhadhiri wa Uandishi wa Habari anasema:
"Kuna habari nyingi ambazo zimehifadhiwa kutoka kwa waandishi wa habari, na
ripoti nyingi kwa hiyo zinatokana na uvumi. Na hapo ndipo habari za uwongo
huingia. Lazima uendelee kushinikiza sheria ambazo zitahakikisha upataji wa
habari. Nchini Cameroon, katiba inatoa fursa hiyo, lakini bado hatuna unamna
ya kupata Sheria ya Habari."
Njodzeka Danhatu, Ripota anaeleza kuwa: Kuongezeka kwa mitandao ya kijamii kumesababisha kuongezeka kwa taarifa potofu nchini Cameroon, na kufanya ukaguzi wa ukweli kuwa kazi ngumu kwa waandishi wengi wa habari. Bado, waandishi wa habari wanasema wanabaki kujitolea kushughulikia athari mbaya za kuenea kwa habari za uwongo."
Kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya kijamii kumesababisha kuongezeka
kwa taarifa potofu nchini Cameroon, na kufanya ukaguzi wa ukweli kuwa kazi
ngumu kwa waandishi wengi wa habari. Bado, waandishi wa habari wanasema
wanabaki kujitolea kushughulikia athari mbaya za kuenea kwa habari za uwongo.
Ripoti ya Njodzeka Danhatu wa VOA, Buea, Cameroon.