Madagascar: Wananchi wadai kura itamaliza mgogoro wa kisiasa

Madagascar inapiga kura katika uchaguzi muhimu wa urais Jumatano ikiwa ni juhudi ya kumaliza mgogoro wa kisiasa na ghasia za miezi kadhaa nchini humo.

Kunawagombea 36 wa kiti cha urais ambapo marais watatu wa zamani wanaoongoza katika duru ya kwanza, kulingana na utafiti wa maoni, lakini ni washindi wawili wa kwanza ndio watapambana katika duru ya pili hapo Disemba 19.

Matarajio ya wananchi

Kwa mujibu wa vyombo vya habari wapiga kura walijitokeza kwa wingi Jumatano kupiga kura katika uchaguzi huo ambao unatarajiwa kutaleta mabadiliko makubwa yatakayo leta ajira na kupunguza hali ya umaskini .

Akizungumza baada ya kupiga kura Jumatano Rais anaetetea nafasi yake Hery Rajaonarimpianina katika mji mkuu wa Antananarivuo alisema ana matumaini zoezi hilo litaleta amani nchini mwake.

"Nina uhakika kwamba hii leo sote tutafanya kila tunalo weza kuleta Amani, na utakuwa ni ushindi kwa ajili ya kuleta amani na demokrasia na heshima kwa wananchi wa Madagascar.

Wagombea urais 36

Miongoni mwa wagombea 36 wanaofahamika zaidi na kuongoza katika utafiti wa maoni ni marais watatu wa zamani Marc Ravalomanana mwenye umri wa miaka 68 aliyechukuwa madaraka 2002 na kulazimika kuacha madaraka februari 7 2009 kutokana na mapinduzi ya wananchi, yaliokuwa yanaungwa mkono na wanajeshi.

Andry Rajolina aliyechukua madaraka kutokana na mapinduzi ya umma ya 2009 na rais anaetetea kiti chake kwa mara nyingine Hery Rajaonarimampianina alichukuwa madaraka mwaka 2013. Hata katiba ya Madagascar wagombea kiti cha urais ajiuzulu kabla ya kugombania nafasi ya urais.

Kuna wapiga kura milioni 10 wanaoweza kushiriki katika uchaguzi ambao utafikisha kikomo mvutano wa kisiasa na ghasia zinazodaiwa kuwa zilizosababishwa na rais anaegombania nafasi yake katika kujaribu kubadili katiba mapema mwaka 2018, ili kuwazuia marais wa zamani kutoweza kushiriki katika uchaguizi.

Wakazi wafurahia kufanyika uchaguzi

Mpigaji kura mmoja aliyehojiwa amesema amefurahi atapiga kura na "ni lazima nipige kura nimekua kimya hadi sasa nitaweza kueleza maoni yangu kwa kupiga kura na tunataka mabadiliko."

Kiongozi kijana Rajoelina, mwenye umri wa miaka 44, anaongoza katika uchunguzi wa maoni anasema ataleta mageuzi katika kupambana na rushwa iliyokithiri, kubuni ajira kuleta manedeleona kurudisha usalama nchini.

Andry Rajoelina Rais wa zamani wa Madagascar : "Wamadagascar wanaishi katika hali ya kukata tamaa na mimi niko hapa kuwaletea matumaini kwa mara nyingine tena. Na tutarekebisha maendeleo yaliyokwama."

Kutokana na katiba ya Madagascar mshindi wa uchaguzi wa rais anahitaji zaidi ya asili mia 50 za kura na kutokana na idadi ya wagombea kutakuwepo na duru ya pili hapo disemba 19.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa kabla ya Novemba 20 na kuthibitishwa na mahakama kuu hapo Novemba 28, 2018.