Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Ijumaa amemteua waziri mkuu mpya Francois Bayrou, kiongozi wa chama cha mrengo wa kati baada ya mazungumzo magumu ili kumpata mrithi wa Michel Barnier aliyeondolewa na bunge wiki iliyopita, Ikulu ya Ufaransa imetangaza.
“Rais wa Jamhuri amemteua Francois Bayrou kama waziri mkuu na amempa jukumu la kuunda serikali”, kulingana na taarifa ya Ikulu ya Ufaransa.
Rais wa chama cha mrengo mkali wa kulia Jordan Bardella, ambaye kura za wabunge wa chama chake zilichangia kwa kumuangusha Michel Barnier amesema chama chake hakitowasilisha hoja ya kumpinga Bayrou.
Bayrou mwenye umri wa miaka 73, atakuwa na kibarua kigumu cha kuunda baraza la mawaziri ambalo halitapingwa na bunge na atakuwa na changamoto ya kupitisha bajeti ya serikali yam waka 2025.