Maafisa hao wamewasili karibu mwezi mmoja baada ya kikosi cha kwanza cha polisi 200 kutuwa katika mji mkuu wa Port-au-Prince, ambako magenge yanadhibiti angalau asilimia 80 ya mji huo.
Mamlaka zimekataa kutoa maelezo kuhusu majukumu ya maafisa hao wa Kenya, zikitaja sababu za kiusalama, ingawa wanahabari wa shirika la habari la AP waliwaona wakishika doria katika maeneo karibu na uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa, ambao ulifunguliwa tena mwishoni mwa mwezi Mei baada ya ghasia za magenge kulazimisha kuufunga kwa karibu miezi mitatu.
Polisi zaidi wa Kenya wanatarajiwa kuwasili katika wiki na miezi ijayo na watashirikiana na polisi na wanajeshi kutoka Bahamas, Bangladesh, Barbados, Benin, Chad na Jamaica wapatao 2,500.
Watapelekwa huko kwa awamu kwa gharama ya dola milioni 600 kwa mwaka, kulingana na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.