Kombora la Russia Jumatano liliua wakazi 9 na kuharibu majengo na miundombinu ya mji wa kaskazini mwa Ukraine wa Chernihiv, maafisa wa mji huo walisema.
Kaimu Meya wa mji Oleksandr Lomako alisema milipuko mitatu ilitokea kwenye sehemu ya shughuli nyingi baada ya saa tatu asubuhi majira ya huko na kuharibu jengo la ghorofa nyingi.
Lomako ameiambia televisheni ya Ukraine “ Kwa bahati mbaya, Russia inaendelea kujihusisha na harakati za kigaidi dhidi ya raia na majengo ya raia kama ilivyothibitishwa katika shambulio hilo dhidi ya Chernihiv kwa mara nyingine.”
Alisema majengo mengi , miundombinu ya kijamii, na magari mengi ya watu binafasi yaliharibiwa.
Gavana wa mkoa Vyacheslay Chaus alisema watu tisa waliuawa na zaidi ya 20 kujeruhiwa.