Kipchoge aweka rekodi mpya ya dunia

Washindi wa Berlin Marathon 2018, Eliud Kipchoge (Kati), Amos Kipruto of Kenya (kushoto) na Wilson Kipsang of Kenya (kulia) wakiwa Berlin, Ujerumani Septemba 16, 2018.

Mwanariadha maarufu wa Kenya Eliud Kipchoge ameweka rekodi mpya ya mbio za mwaka 2018 za Berlin Marathon, ambapo Kenya pia imeongoza nafasi tatu za mwanzo.

Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa mwanariadha huyo ambaye anakimbia mbio za masafa marefu kwa kasi zaidi, mwenye umri wa miaka 33, ametumia saa 2, dakika 6 na sekunde 39 kwa kumaliza kilomita 42.

Kipchoge ameipiku rekodi aliokuwa ameiweka Dennis Kimetto wa Kenya ya saa 2, dakika 2 na sekunde 57 katika mbio kama hizo zilizo kuwa zimefanyika Berlin 2014.

Hii itakuwa mara ya tatu kwa Kipchoge kutwaa ushindi katika mbio hizo za Berlin Marathon.

Ushindi wa pili umechukuliwa na mwanariadha wa Kenya Amos Kipruto aliyetumia saa 2, dakika 6 na sekunde 24 katika mbio hizo. Nafasi ya tatu amechukuwa Wilson Kipsang Mkenyaaliyekimbia kwa saa mbili, dakika sita na sekunde 48.

Mbio za Berlin Marathon zimeshuhudia mshindi mwanamke kutoka Kenya Gladys Cherono ambaye ameendelea kuwa mshindi tena kwa kutumia saa 2, dakika 18, na sekunde 11.

Kwa upande wa Ethiopia wanariadha wake Ruti Aga na Tirunesh Dibaba walimaliza wikiwa namba mbili na namba tatu katika mbio hizo.