Mahakama nchini Guinea Jumatano ilimuhukumu kiongozi wa zamani dikteta Moussa Dadis Camara kifungo cha miaka 20 jela kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, baada ya kesi ya kihistoria kuhusu mauaji ya mwaka 2009 katika mkutano wa kisiasa.
Washtakiwa wengine saba walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani mwishoni mwa kesi iliyosikilizwa kwa zaidi ya karibu ya miaka miwili, katika hukumu iliyopongezwa na wanaharakati wa haki za binadamu.
Maafisa wa usalama walikuwa wamepelekwa kwa wingi wakati kesi hiyo ikisikilizwa, kesi ambayo ilisubiriwa kwa hamu na familia za waathirika kwa karibu miaka 15.
Mahakama iliamuru pia waathirika walipwe fidia, kuanzia milioni 200 hadi bilioni 1.5 faranga za Guinea.