Kiongozi wa upinzani Zimbabwe ahukumiwa jela kwa kumtukana raia wa Russia

  • VOA Swahili

Kiongozi mkuu wa upinzani wa upinzani Zimbabwe Tendai Biti akiwasili mahakamani mjini Harare Agosti 9, 2018.

Mahakama nchini Zimbabwe imemhukumu kiongzi wa upinzani kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya dola 300 kwa tuhuma za kumtukana mfanyabiashara wa kike kutoka Russia

Hakimu Vongai Guwuriro aliamua kwamba Tendai Biti, waziri wa fedha wa zamani wa Zimbabwe, anabidi alipe faini au aende jela, na hivyo kumaliza ugomvi wa miaka minne uliokuwa mahakanani kati ya Biti na Tatiana Aleshina, ambae hati za mahakama zinaonesha ni mwekezaji kutoka Russia.

Alec Muchadehama, wakili wa Biti amewaambia waandishi wa habari nje ya makahama ya hakimu mkazi ya Harare siku ya Jumanne kuwa Biti atakata rufaa dhidi ya kifungo na hukumu hiyo.

Mwendesha mashitaka wa serikali amemshutumu Biti kwa kumuita Aleshina “mpumbavu” na kumnyoshea kidole mwaka 2020. Biti alikana mashitaka ya kumshambulia kwa maneno.

Aleshina amesema hukumu hiyo ni ushindi kwa wanawake.

Wafuasi wa Aleshina waliokuwa nje ya mahakama walisema Biti alistahili kutopewa nafasi ya kuchagua kati ya kulipa faini au kupelekwa jela, wakati wafuasi wa Biti wakisema adhabu kwa ajili ya kumuita mtu “mpumbavu” si haki

Biti ni makamu rais wa chama kikuu cha upinzani cha Citizen Colition for change.