Kimbunga Harvey kimeimarika wakati kikisafiri kwenye maji yenye uvuguvugu katika ghuba ya mexico, kikielekea kwenye pwani ya texas.
Watabiri wa hali ya hewa wa marekani wanasema harvery kitakuwa kimbunga kikubwa kitapofika katike eneo hilo Ijumaa jioni.
Upepo mkali tayari umefikia kasi ya kilometa 177 kwa saa ikiwa imebaki kiwango kidogo tu kutajwa kuwa ni dhoruba ya daraja la tatu.
Upepo huo unatarajiwa kuvuka kilometa 200 kwa saa wakati kimbunga kitapopiga mwambao wa ukubwa wa kilometa 600.
Mkuu wa idara ya majanga ya serikali kuu ya marekani ameonya hivi leo kuwa maafa makubwa yatalipiga eneo la texas.