Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, mkutano na waandishi wa habari ambao ulitangazwa moja kwa moja kwa taifa ulikuwa ni maoni ya kwanza kutoka kwa kikosi cha Kenya, ingawa wanahabari hawakupewa nafasi ya kuuliza maswali.
Godfrey Otunde, ambaye ni afisa wa Kenya anayeongoza ujumbe huo amesema kuwa, “Tunanuwia kuanikisha hili kwa kufanya kazi kwa karibu sana mamlaka za Haiti, pamoja na washirika wa kitaifa na kimataifa, wenye nia ya kuiona Haiti mpya.
Ujumbe huo unaoungwa mkono na UN, na ambao Marekani imeahidi kutoa dola milioni 300, uliibua maswali tangu mwanzoni. Nchini Kenya polisi wamekuwa wakilalamikiwa na wanaharakati pamoja na mashuhuda kukiuka haki za binadamu, ikiwemo kwenye maandamano ya hivi karibuni.